Chama cha Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini, kimeadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwenye Mnara wa Shule ya Msingi Bugoyi A Mjini humo, ambapo siku anafariki dunia Mwenge wa uhuru ulikuwa shuleni hapo.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Oktoba 14, 2019, siku ambayo alifariki Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999, akiwa nchini London akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Mtakatifu Thomas ambapo imepita miaka 20 sasa.
Akizungumza mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu, amewataka vijana hao wa Skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo, kwa kuwa wazalendo kuipenda nchi yao pamoja na kudumisha amani na upendo.
Amesema zawadi pekee ambayo vijana hao wanapaswa kumpatia Mwalimu Nyerere, ni kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani ya nchi ambayo aliiacha Baba wa Taifa, na siyo kumuenzi kwa kutenda mambo mabaya ikiwamo kujiingiza kwenye madawa ya kulevya.
“Vijana ni taifa la kesho hivyo nyie kama Skauti ambao mnapitia mafunzo mengi, mnapaswa kwenda kueneza elimu kwa vijana wenzenu ya kuwa wazalendo na kuipenda nchi, pamoja na kudumisha amani na upendo vitu ambavyo ametuachia Baba yetu wa Taifa,”amesema Mkadamu.
“Pia na waomba na wanafunzi kote nchi mumuenzi Baba yetu wa Taifa kwa kusoma kwa bidii na kumfukuza Adui ujinga, moja ya maadui watatu aliokuwa akiwapinga, na kuachana na tabia ya kwenda na simu shuleni na kuanza kuchati na kuwasababishia kufanya vibaya kimasomo,”ameongeza.
Naye Katibu wa Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini Vicent Kanyogoto, amesema wamedhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwenye mnara huo, ambapo wamekaa muda wa siku nne kwa wakifanya shughuli za usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti na kuwapatia vijana elimu ya uzalendo pamoja na kudumisha amani na upendo.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu akizungumza kwenye kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, maadhimisho yaliyofanyika kwenye Mnara wa Shule ya Msingi Bugoyi A, na kuwataka vijana kumuze Nyerere kwa kuwa wazalendo katika nchi. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu, akitoa wito kwa wanafunzi kumenzi Mwalimu Nyerere kwa kusoma kwa bidii na kumfukuza adui ujinga.
Mjumbe wa Kamati ya Ufuatiliaji na Hamasa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Eric Daudi akiwaasa vijana wa Skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kudumisha amani na upendo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Ndembezi Pendo John akitoa nasaha kwa vijana hao wa skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kutenda mambo mazuri .
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A, Anna Alute akipongeza vijana hao wa Skauti namna walivyoboresha mazingira ya usafi shuleni hapo ukiwamo na mnara huo wa Mwalimu Nyerere pamoja na kupanda miti.
Mwanafunzi Emmanuel Barnaba anayesoma Shule ya Msingi Bugoyi A akisoma risala ameiomba Serikali kuboresha miundo mbinu ya Shule hiyo, ilikuendana na hadhi ya Mnara wa kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere.
Katibu wa Chama cha Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini Vicent Kanyogota akizungumza kwenye maaadhimisho hayo ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Nyerere, kwenye Mnara wa Nyerere uliopo shule ya Msingi Bugoyi A.
Skauti wakiwa kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwenye Mnara wa Nyerere katika shule ya Msingi Bugoyi A, ambapo siku Mwl .Nyerere anafariki Mwenge wa uhuru ulikuwa Shuleni hapo.
Skauti wakiwa kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwenye Mnara wa Nyerere katika shule ya Msingi Bugoyi A.
Mafundi wakiendelea kujenga Mnara wa kumbukumbu wa Mwalimu Nyerere katika shule ya Msingi Bugoyi A, ambapo siku anafariki dunia, Mwenge wa Uhuru ulikuwa shuleni hapo na ulizimwa mara baada ya kutangazwa kwa kifo chake na kupelekwa kanisani.
Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mukadamu akipanda mti kwenye Shule ya Msingi Bugoyi A, MahaLi ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere.
Kamishina wa Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini, Peter Mgalula akipanda Mti kwenye shule ya Msingi Bugoyi A, Mahari ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere.
Katibu wa Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini, Vicent Kanyogoto akipanda Mti kwenye shule ya Msingi Bugoyi A, Mahari ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A, Anna Alute akipanda mti.
Vijana wa Skauti nao wakipanda miti.
Vijana wa Skauti wakijipanga tayari kwa kufanya maandamano kuzunguka mjini Shinyanga huku wakiwa wameshika picha ya Mwalimu Nyerere.
Vijana wa Skauti wakijiandaa kufanya maandamano huku pia wakibeba picha ya Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufuli.
Vijana wa Skauti wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwa kuzunguka mitaa ya mji wa Shinyanga.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea na burudani ikiendelea.
Awali Mgeni Rasmi Kwenye maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Nyerere Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga akivalishwa skafu mara baada ya kuwasili kwenye Mnara wa Mwalimu Nyerere katika Shule ya Msingi Bugoyi A.
Skauti wakitoa burudani ya kucheza Kwaito wimbo wa Tanzania Tanzania.
Vijana kutoka kundi la The Fire mjini Shinyanga nao wakitoa burudani.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu akihitimisha maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwa kugawa vyeti kwa wahitimu wa Skauti.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa hitimu wa Skauti.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa hitimu wa Skauti.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa hitimu wa Skauti.
Skauti wakipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwamo Afisa elimu wa shule za msingi manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga katikati mwenye kilemba kichwani pamoja na viongozi wao wa Skauti.
Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog