Home Mchanganyiko OSHA yawafunda wakaguzi wake

OSHA yawafunda wakaguzi wake

0

 Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank Mwaisumbe akifungua mafunzo ya Usalama na Afya Jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. frank Mwaisumbe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya OSHA.

Kaimu Mtendaji Muu wa OSHA Bi Khadija Mwenda akizungumza wakati wa mafunzo hayo jijini Arusha.

Baadhi ya  washiriki wa mafunzo ya usalama na Afya Mahali Pa kazi wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo hayo.

*************************

Mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Frank Mwaisumbe amewapongeza OSHA kwa
kubadili mfumo wa utendeji kazi wake na kuondoa urasimu wa utendaji kazi,
kwani urasimu hupelekea shughuli nyingi kukwama, na hivyo wawekezaji wengi
kukimbia nchini kuwekeza kutokana na kuwepo na vikwazo.

Ndugu Frank ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa Arusha Mhe. Mrisho Gambo,
amesema hayo leo jiji Arusha wakati ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa Usalama na Afya toka OSHA na WCF,amesema juhudi za kupunguza TOZO kumeisaidia OSHA kuweza kuwafikia wawekezaji wengi zaidi na hivyo suala la Usalama na Afya Mahali Pa kazi kuanza kutekelezwa na kuzingatiwa na waajiri wengi hapa nchi.

“Nimefarajika kusikia kwamba, mmendelea kuboresha huduma zenu, hilo ni
jambo jema .Waajiri wengi nchini hawatapendi kuona urasimu, kwani wengi wao
wawekezaji wakiona kuna urasimu huondoka na kutafuta sehemu zingine ili
waweze kuwekeza” Mhe. Mwaisumbe alieleza.

Mkuu huyo wa wilaya alisema juhudi hizi ambazo zimefanywa na OSHA pamoja na mafunzo hayo, yamekuja kipindi kizuri, Hasa kipindi hiki nchini yetu inapotekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama vile miradi ya Umeme,ujenzi wa Barabara, madaraja, na hivyo miradi hii huajiri watu wengi, hivyo mafunzo kama haya yatawaweza kuwapatia mbinu zaidi wakaguzi wanapotekeleza majukumu yao.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi Khadija Mwenda amesema mafunzo hayo
yameandaliwa kwa lengo la kuwaongezea uwezo watumishi wa Umma kwa lengo la kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi. Kwani kwasasa Wakala
unaendelea kuboresha huduma zake, hivyo mafunzo hayo yataongeza ufanisi kwa wakaguzi wawapo kazini.

Khadija amesema yakuwa wakati nchi inaendelea kupiga hatua mbalimbali za
kiuchumi na mabadiliko mbalimbali ya Kiteknolojia duniani, hivyo mafunzo kama haya yatakuwa muafaka kwani yataenda sambasamba na kuwafunza wakaguzi
mbinu mpya za kukabiliana na mabadiliko hayo pamoja na changamoto.

“ Wenzetu hawa huko kwao masuala ya usalama na Afya yanazingatiwa na
yanapewa kipaumbele, sasa ujuzi ambao wakaguzi wataupata kutoka kwa
wataalamu hawa yatasaidida kuboresha utendaji kazi wetu, na mbinu mpya za
kuweza kufanikisha zoezi zima la kufanya kaguzi za usalama na Afya

Naye ndugu Aristides Medard mjumbe wa shirika la Workplace Health without
Borders (WHWB) toka Tanzania ambao ni waratibu wa mafunzo hayo kwa
kushirikiana na OSHA kwa upande wa Tanzania amesema lengo kubwa la taasisi
hiyo ni kuhakikisha linatoa mafunzo yanayolenga kuondoa changamoto
mbalimbali za usalama na Afya Mahali pa kazi duniani ambazo hujitokeza.

Mafunzo haya ya wiki moja yameandaliwa na OSHA kwa lengo la kuwajengea
uwezo wa wakaguzi wa OSHA pamoja na WCF, namna bora ya kufanya kaguzi, na yanaendeshwa na wakufunzi kutoka CANADA,MAREKANI na UBELGIJI kutoka
shirika la kimataifa la Workplace health without Border (WHWB).