Home Mchanganyiko SERIKALI KULIPA MIL 315.1 ZA WAKULIMA WA MUZIA AMCOS MKOANI RUKWA –...

SERIKALI KULIPA MIL 315.1 ZA WAKULIMA WA MUZIA AMCOS MKOANI RUKWA – MHE HASUNGA

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa jana tarehe 13 Octoba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joachim Wangabo na mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe Julieth Binyura. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wawakilishi wa Wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitatua kadhia za chama hicho kuhusu kutapeliwa fedha na Mwenyekiti wa chama hicho Ndg Linus Kalandamwazye kiasi cha Shilingi Milioni 315.1 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joachim Wangabo na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe Julieth Binyura wakijadili jambo mara baada ya kumalizika kikao kazi kuzungumza na wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa jana tarehe 13 Octoba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa, Kulia kwake ni 
Sehemu ya wawakilishi wa Wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitatua kadhia za chama hicho kuhusu kutapeliwa fedha na Mwenyekiti wa chama hicho Ndg Linus Kalandamwazye kiasi cha Shilingi Milioni 315.1 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.
 
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Rukwa
 
Serikali imetangaza dhamira
yake ya kuwalipa wakulima 156 wa mahindi jumla ya Shilingi 315,118,510 kutokana
na kuzulumiwa na mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ndg Linus Kalandamwazye.
 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga ametoa kauli hiyo jana tarehe 13 Octoba 2019 wakati akizungumza na
wanachama wa Muzia Amcos Wilayani Kalambo wakati akiwa katika ziara ya kikazi
ya siku moja mkoani Rukwa.
 
Malipo hayo yatawahusu
wakulima wa Tarafa ya Mwimbi yenye kata nne ambazo ni Mambwe Kenya, Ulumi,
Mkombo na Mwazye kutokana na kupima mahindi yao zaidi ya Tani 622.679 kwenye
Chama cha Muzia Amcos kilichopewa uwakala na serikali wa kununua mazao kwa
wakulima tarehe 8 Agosti 2017 kwa makubaliano ya kulipwa ndani ya wiki tatu
kutoka tarehe ya kupimwa lakini hawakulipwa mpaka sasa.
 
“Kesi ikiwa mahakamani
serikali haiwezi kuingilia badala yake wakati tunaendelea na kesi hiyo
ninaziagiza taasisi zangu tatu kuchanga fedha kwa ajili ya kuwalipa wakulima
hao” Alikaririwa Mhe Hasunga
 
Alisema wanaotakiwa kuchanga
fedha hizo kwanza ni Wizara ya Kilimo kwa kushindwa kulishughulikia jambo hilo
kwa wakati ili wakulima hao waweze kulipwa fedha zao.
 
Ameiagiza pia Tume ya
Maendeleo ya Ushirika kuchanga fedha hizo kwani wao ndio wasimamizi wa Vyama
vya Ushirika lakini kwa kipindi chote wameshindwa kushughulikia changamoto hiyo
ya wakulima.
 
Kadhalika, Mhe Hasunga Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kuchangia fedha hizo.
 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt
John Pombe Magufuli haina dhamira ya kuwadunisha na kuwafedhehesha wananchi
badala yake imejipambanua kuwanufaisha wakulima katika kilimo.
 
Alisema kuwa serikali imeamua
kuwalipa fedha hizo wakulima ili kuendelea na uzalishaji bora wa mazao ya
kilimo lakini kesi itakapomalizika serikali itazidai fedha hizo.
 
Mhe Hasunga amemuagiza
Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Rukwa kupanga vizuri madai ya wakulima hao huku
akisisitiza kutoingizwa majina mapya (Majina Hewa) yasiyohusika na madai ya
fedha hizo.
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mhe Joachim Wangabo amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwa
kukubali kulivalia njuga jambo hilo kwa kuwalipa fedha hizo wakulima kwani
kufanya hivyo kutarahisisha wakulima hao kuendelea na uzalishaji wa mazao
katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020.
 
Amesema kuwa maamuzi hayo ya
wizara kuamua kuwalipa wakulima huku taratibu zingine za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuchukuliwa hatua Mwenyekiti huyo zikiwa zinaendelea zimeibua ari na
nguvu mpya katika kilimo.
 
Awali, akisoma taarifa ya
malalamiko ya kutapeliwa fedha hizo katibu wa chama cha MUZIA AMCOS Ndg Geofrey
Mbati amesema kuwa pamoja na kupeleka malalamiko katika maeneo mengi lakini
ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wa karibu katika
kipindi chote cha kutafuta muarobaini wa malipo ya wakulima.
 
Alisema kuwa miongoni mwa
maoni ya wakulima ilikuwa ni ombi la kupatiwa fedha hizo kwa ajili ya
kuwanusuru kutokana na kadhia hiyo ya muda mrefu iliyopelekea kushindwa kulipa
ada za wanafunzi shuleni, kushindwa kuwekeza tena kwenye kilimo pamoja na
kushindwa kumudu gharama za maisha hali iliyopelekea kuishi maisha ya kifukara.