Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akikagua Ujenzi wa Daraja wenye urefu wa Kilomita 66.9, ambao umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 105 akikagua ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara .
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Wananchi Katika Eneo la Ujenzi wa Daraja wenye urefu wa Kilomita 66.9, ambao umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 105 akikagua ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara .
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndg. Sophia Mjema akizungumza na Wananchi waliofika Katika Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo wakati wa Ukaguzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja wenye urefu wa Kilomita 66.9, ambao umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 105 akikagua ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara .
Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjemaakizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wakulima wa miwa kata ya Asanje Wilayani Kilombero katika ziara yake mkoani Morogoro ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua uhai wa chama na kukiimarisha ngazi ya mashina.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM )
Katibu wa Idara ya Oganaizeshen CCM Ndg. Issa Gavu akizungumza na Wananchi waliofika Katika Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo wakati wa Ukaguzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja wenye urefu wa Kilomita 66.9, ambao umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 105 akikagua ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara .
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Wananchi pamoja na Wanachama wa CCM katika Kijiji Cha Kibelege waliomsimamisha kumsikiliza akiwa njiani kuelekea mji wa ifakara wakati wa ziara yake mkoani Morogoro ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua uhai wa chama na kukiimarisha ngazi ya mashina.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM )
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo Pichani akiwa na wananchi wakulima wa miwa kata ya Asanje Wilayani Kilombero na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Taifa wakati wa ziara yake mkoani Morogoro ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua uhai wa chama na kukiimarisha ngazi ya mashina.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM )
……………………………………….
Wakulima wa miwa wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamelalamikia kukosa imani Kiwanda cha Sukari Kilombero kwa jinsi wanavyopima kiwango cha utamu wa miwa wauzayo kiwandani hapo ambayo hupewa malipo madogo kwa madai utamu uko kiwango cha chini.
Malalamiko hayo yametolewa leo tarehe 31 Januari, 2023 wilayani Kilombero na wananchi wakulima wa miwa mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akiendelea na ziara yake mkoani Morogoro ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua uhai wa chama na kukiimarisha ngazi ya mashina.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kilombero, Mbunge wa Kilombero Abobakar Assenga amesema changamoto kubwa ni mgogoro baina ya wakulima wa miwa na kiwanda cha Kilombero.
“mgogoro mkubwa ni kiwango cha utamu wa mua (Sucrose), malipo ya mkulima anayekwenda kuuza miwa yake kiwandani hapo yanategemea utamu wa mua, sasa wakati wa kupima hakuna mkulima anayepewa fursa ya kujua bali anaambiwa utamu wa mua ni mdogo na malipo yanakuwa madogo”,amesema Assenga.
Amesema mgogoro huo ni wa muda mrefu na viongozi wengi wamepita lakini tatizo liko palepale.
Akizungumzia kero na malalamiko hayo, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kutengeneza utaratibu wa kukaa na Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Biashara(Amcos) viteue wakulima mmoja mmoja wafundishwe jinsi ya kufahamu upimaji wa kiwango cha utamu wa sukari ili kuondoa manung’uniko yao.
Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akiwa ameongozana na na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu).