Tanzania imesisitiza kuwa uwekezaji kwa watoto ni uwekezaji katika uchumi, maendeleo endelevu na mustakabali wa taifa.

Ujumbe huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu — Sera, Bunge, Uratibu na Watu wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, anayemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kongamano la Amani la Paris, tarehe 10–11 Novemba 2026.

Akichangia mjadala wa ngazi ya juu kuhusu uwekezaji kwa watoto, Prof. Kabudi ameeleza kuwa Tanzania inaunga mkono Azimio la “Watoto Kwanza”, akitoa wito wa kutafsiri ahadi kuwa bajeti, huduma bora na matokeo yanayopimika.

Ameangazia mafanikio ya Tanzania, ikiwemo kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano kwa asilimia 36 kati ya mwaka 2015/16 na 2021/22, huku akisisitiza kuongeza uwekezaji katika afya, lishe na ulinzi wa watoto.

Katika kongamano hilo, Prof. Kabudi amepata fursa ya kuonana na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal. Pia ameshiriki mjadala wa ngazi ya juu ulioongozwa na Rais Macron na kuwashirikisha wakuu wa taasisi za Umoja wa Mataifa kuhusu ustawi wa watoto duniani.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ni kila mtoto anastahili nafasi ya kuishi, kukua na kutimiza ndoto zake.