Timu ya kamba ya Bunge wanaume 

 Katika Mchezo mwingine Bunge nao wamejikatia
tiketi ya kucheza 16 bora baada ya kuwavuta Wizara ya mambo ya nje kwa mivuto
miwili.

 Matokeo ya jumla ya kundi E ni Uchaguzi alama 9,
Bunge alama 8 na Wizara ya Mambo ya Nje alama 7 hivyo timu za Uchaguzi na Bunge
wamefuzu kucheza hatua ya pili ya mashindano ya SHIMIWI 2022.
 
Kwa matokeo hayo sasa Uchaguzi wanaume inayoongoza
kundi E itakutana na Wizara ya Elimu wakati Uchaguzi wanawake kutoka Kundi F itakutana
na Wizara ya Katiba na Sheria.