Oktoba 1, 2019 kutakuwa na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuzaliwa taifa la Jamhuri ya Watu wa China. Maadhimisho hayo yamepewa uzito mkubwa na yatajumuisha matukio mbalimbali ikiwemo Gwaride kubwa ambalo halijawaji kutokea hapa China. Vilevile wataonesha hatua kubwa waliyopiga ndani ya kipindi cha miaka 70 katika sayansi na teknolojia pamoja na nguvu za kijeshi. Katika ku revisit safari yao ya miaka 70 wameutambua mchango wa Tanzania katika maeneo mawili. Moja- mchango wa kuwawezesha kupatiwa kiti katika Umoja wa Mataifa na pili fursa waliyopata kutekeleza mradi wa kwanza wa ujenzi wa Reli nje ya nchi (TAZARA).
Katika kutambua mchango wa Tanzania kuwawezesha kuingia UN- Rais wa China Mhe Xi Jinping atamtunuku Mhe Dr. Salim Ahmed Salim Nishani ya Juu ya Urafiki ya taifa la China. Dr Salim atakuwa Mwafrika wa kwanza kupatiwa nishani hiyo na mtu wa tatu kutoka nje ya China kupatiwa nishani hiyo. Wengine waliokwishapatiwa nishani hiyo ni Rais wa Urusi Mhe Vladmir Putin- kutokana na mchango wa mkubwa wa Urusi kwa taifa la China katika miaka 1949-1970… waliwapa mikopo nafuu, mitaji, teknolojia na ufundi iliyowawezesha kupiga hatua. Pia nishani hiyo amewahi kupewa Kiongozi wa Khazakstan Mhe
DescriptionNursultan Äbishuly Nazarbayev kutokana na ujirani mwema na ushirikiano mkubwa katika nyanja za ulinzi na uchumi. Khazakstan inapakana na China (mpaka wao una urefu wa kilomita 1,782.75). Mizigo ya China inayosafirishwa kwenda Ulaya kwa treni, lazima ipitie Khazakstan- hiyo nchi hiyo ni strategic country kwa China.
Kwa upande wa mchango wa Reli ya TAZARA wachina wanaichukulia kuwa ni alama ya urafiki kati ya China na Bara la Afrika. Hivyo katika kutambua urafiki huo- viongozi wa taasisi za China-Tanzania Friendship Association na Tanzania Zambia Friendship Association wamealikwa kuhudhuria sherehe za miaka 70 na pia watashiriki katika gwaride rasmi la Nchi Rafiki wa kweli wa China katika kipindi cha miaka 70. Kutoka Afrika ni nchi mbili tu- Tanzania na Zambia.