……………….
Na Sixmund Begashe wa MNRT
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe Yuri Pimentel Moura kwa lengo la kuimarisha mahusinao katika Sekta ya Maliasili na Utalii kati ya Tanzania na Venezuela.
Kikao hicho kilichofanyikia Jijini Dar es Salaam kimeudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi na wataalam wa Wizara za nchi zote mbili.