Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania unaohudhuria Mkutano Mkuu wa 63 wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Maryam Juma Abdulla, akiwasilisha taarifa kwa niaba ya serikali ya Jumhuri ya muungano wa Tanzania kwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo (hawapo pichani) leo mjini Vienna-Austria.
Katika Taarifa yake Mh. Katibu Mkuu aliishukuru IAEA kwa kuendelea kusaidia juhudu za Serikali katika kuboresha sekta mbalimbali zikiwemo sekta ya Afya, Kilimo, Mifugo, Lishe, Maji nk. Awali Mh. Katibu Mkuu aliwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Ndugu Yukiya Amano kilichotokea mapema mwezi Julai 2019.