Mbunge Zaynabu Matitu Vullu akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Dimani Wilaya ya Kibiti
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani,Mh Zaynabu Matitu Vullu akikagua majengo ya Zahanati ya Dimani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa chama Cha Mapinduzi (UWT), Zaynabu Matitu Vullu akiwaeleza Wanawake wa wilaya ya Kibiti juu ya Umuhimu wa Bima ya Afya.
…………………………………………………..
Na Mwandishiwetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa chama Cha Mapinduzi (UWT) ,Zaynabu Matitu Vullu amewaomba Wanawake wa wilaya ya Kibiti kucheza Upatu wa kununulia bima za Afya na sio vyombo.
Mh Zaynabu amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanawake wa wilaya hiyo kwenye ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM Kibiti.
“Mimi nawaomba Wanawake wenzangu tuache kutunza vyombo badala yake tutunzane kadi za CHF Iliyoboreshwa hili tuweze kupunguza gharama za matibabu pindi tunapougua au kuuguliwa ndani ya familia” amesema Mh Zaynabu.
Amewaeleza kuwa Kama Kila mmoja atauza kuku wawili nakujipatia bima kwa gharama ya Shilingi 30,000 ambayo itaweza kutibia watu sita ndani ya familia moja ambao Ni Baba,Mama na wategemezi wanne.
Amesema matumizi ya Bima yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini usiokuwa wa lazima kwa kuokoa gharama za matibabu .
Aidha ametaja kuwa matumizi ya Bima yanapunguza presha pindi Mama anapokuwa mjamzito pindi unapofija wakati wa kujifungua kwa kusaidia kupata huduma kwa uhakika.
Pia aliwaomba wamama hao kufikisha ujumbe huo kwa kinababa na waume zao kwani swala la Afya ya familia ni jukumu la kila mmoja wetu.