Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Abubakar Muna (katikati mwenye fulana ya blue) akiwa na Wananchi wa Kijiji cha Masweya baada ya kukagua eneo itakapo jengwa Shule Shikizi ya Kitongoji cha Nsonga Ndogo wilayani Ikungi mkoani Singida.
Ukaguzi wa eneo hilo ukifanyika.
Picha ya pamoja baada ya ukaguzi huo.
Na Dotto Mwaibale,
Ikungi
MBUNGE wa Jimbo la
Singida Magharibi Elibariki Kingu ametembelea eneo la miradi itakapojengwa
Shule Shikizi katika KijijiK cha Masweya Kitongoji cha Nsonga Ndogo
wilayani Ikungi mkoani Singida ambapo aliwakilishwa na Katibu wake
Abubakar Muna.
Katika ukaguzi huo
uliofanyika mwishoni mwa wiki, Muna kukutana na viongozi wa Halmashauri
ya Kijiji cha Masweya na baadhi ya viongozi wa chama kutoka kwenye matawi yote
matatu na kuzingumza nao.
Mazungumzo mkubwa
yaliyofanyika baina yao yalihusu maendeleo ya miradi minne inayotekelezwa
katika maeneo mbalimbali kwenye vitongoji vya Ifyamahumbi ambao wanamradi wa
madarasa mawili yanayoendelea kujengwa.
Akizungumza na
waandishi wa habari Muna alisema miradi yote inayotekelezwa katika maeneo hayo
unakwenda vizuri kutokana na ushirikiano mkubwa wa wananchi na viongozi.
Alisema katika
Kitongoji cha Nsonga Ndogo wana mradi wa Shule Shikizi ambapo walipewa mifuko
100 ya saruji na Mbunge Elibariki Kingu huku Sh. 50 Milioni zikitolewa na Rais
Samoa Suluhu Hassan kwa ajili ya akisaidia ujenzi wa Zahanati ya Kitongoji
hicho.
Alisema ujenzi wa
mradi wa Zahanati wa Kitongoji cha Masweya unaendelea vizuri na umefikia hatua
ya lenta.Nsonga Ndogo iliopewa mil 50 na Mh Rais mama Samia Suluhu Hassan,mradi
wa mwisho ni zahanati ya Masweya ilioko kwenye lenta.
Muna alisema wananchi
wa vitongoji vyote pamoja na viongozi wao wamekubaliana kuendelea na miradi kwa
kuchangia kila kaya ili kuisukuma mbele miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika
ikiwa ni kuunga mkono jitihada za mbunge wao.
Viongozi pamoja na
wananchi wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo wakatumia nafasi hiyo
kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha na pia wakampongeza Mbunge
wao Kingu kwa kazi nzuri huku wakihimiza kudumisha ushirikiano baina yao.