Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid (kulia) akipokelewa na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu alipowasili leo katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akisajiliwa kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho cha Mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika leo katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid (katikati) akiongozana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said (kulia) na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu leo katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akisalimiana na Watumishi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ndg. Raya Issa Mselemo
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
……………….
Na Debora Sanja, Bunge
Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa waliyoipata ya kuwa wenyeji wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kujitangaza kibiashara na kitalii.
Mheshimiwa Maulid ametoa rai hiyo leo Kisiwani Zanzibar wakati akikagua maandalizi ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Agosti hadi septemba 5 mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business & Spa.
Alisema mkutano huo kufanyika Zanzibar utafungua fursa katika sekta za biashara ikiwemo utalii na kuwataka Watanzania kuonyesha ukarimu kwa wageni hao.
“Tuonyeshe ukarimu wakati kupokea wageni hawa, tuitendee haki nchi yetu, tukikaa nao vizuri wageni wetu itatosha kwa sisi kujitangaza, tutumie fursa hii kwa kadri tutakavyoona inaweza kuisaidia nchi” alisema.
Alisema mkutano huo ni wa kihistoria kwa kuwa unaweza kuvunja rekodi ya mahudhurio ya wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchi 18 wanachama ambao unajumuisha maspika, manaibu spika na wabunge.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPA, Tawi la Zanzibar, Mheshimiwa Simai Mohammed Said alisema mkutano huo mbali na kutoa fursa za kiuchumi lakini pia utawezesha wajumbe kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuisimamia Serikali katika mambo yanayogusa wananchi.
Awali akizungumzia maandalizi ya awali, Katibu Msaidizi wa CPA, Kanda ya Afrika, Said Yakubu alisema Nchi zote 18 wanachama zimethibitisha ushiriki na kwamba maspika 23 kutoka mabunge makubwa na madogo watahudhuria.
Alisema nchi wanachama wa CPA, Kanda ya Afrika ni Botswana, Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Siera – Leone, Afrika ya Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.