Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Maharage Chande akikagua ujenzi wa upanuzi wa mtambo wa Kiyerezi 1 utakaozalisha megawati 150 wakati utakapokamilika.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Maharage Chande akifafanua jambo wakati alipokagua ujenzi wa upanuzi wa mtambo wa Kiyerezi 1 utakaozalisha megawati 150 wakati utakapokamilika
Muonekano wa baadhi ya mitambo ambayo tayari imeshafungwa katika mradi huo wa upanuzi wa Kinyerezi 1.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi ya ufungaji wa mitambo katika mradi huo.
Baadhi ya Tabani za kufua umeme zikishushwa kwenye magari makubwa katika eneo la mradi kinyerezi 1.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Maharage Chande akikagua ujenzi wa upanuzi wa mtambo wa Kiyerezi 1 utakaozalisha megawati 150 wakati utakapokamilika katika maeneo mbalimbali ambayo mitambo inafungwa.
……………………………………
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Maharage Chande amesema katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa umeme nchini Shirika hilo limeendelea na maboresho ya vituo mbalimbali vya kufua na kupoza umeme kikiwemo hicho cha Kinyerezi I kitakachozalisha Megawati 185 zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.
Amesema matarajio ni kwamba ifikapo Aprili Mwaka huu, kituo hicho kitaanza kuzalisha Megawati 70 na ifikapo Agosti Mwaka huu kitakamilika na kuanza kuzalisha Megawati 150 na kukifanya kuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 335.
Katika hatua nyingine Mtendaji Mkuu huyo wa Tanesco alisema Shirika hilo linaendelea kufanya maboresho katika vituo vyake vya uzalishaji wa umeme vilivyopo maeneo mbalimbali nchini lengo ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo unakuwa wa uhakika.
Maharage Chande ameyasema hayo wakatialipozungumza na waandishi wa habari alipokuwa akielezea maendeleo ya uboreshaji wa kituo hicho cha Kinyerezi 1 leo jijini Dar es Salaam
ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya umeme inayojitokeza.
Ameongeza kwamba katika kipindi cha uboreshaji huo kutakuwa na maboresho ya mfumo wa uingizaji gesi katika mitambo yake hivyo kusababisha upungufu wa umeme utakaopelekea maeneo mbalimbali kukosa umeme kwa siku 10 kuanzia Februari Mosi hadi 10 mwaka huu.
“Maboresho hayo yanatokana na uhitaji wa kiasi kikubwa cha gesi katika mitambo inayoongezwa mahali hapo na hivyo kuhitaji muda huo kwa wazalishaji hao ambao ni Shirika la Maendeleo ya Petrli Tanzania(TPDC) na Pan African Energy Tanzania(PAET) kufanya maboresho katika visima vya Songosongo kuanzia Februari Mosi hadi 10 Mwaka huu.
Naye Msimamizi wa kituo cha uzalishaji umeme cha Kinyerezi I Abdallah Choyo alisema Uboreshaji wa mitambo hiyo ya uzalishaji umeme kwa kiasi Kikubwa kutasaidia shirika hilo kurudi katika hali ya kawaida katika utoaji huduma wake kwa wananchi .
Alisema hadi sasa maboresho ya mitambo hiyo yamefikia asilimia 85 na hivyo kufanya kazi iliyosalia kuikamilisha kuwa ndogo ikichangiwa na jitihada za kumaliza changamoto ya ukosefu wa umeme inayochukuliwa na Tanesco