…………………………………………………………………

Na.Alex Sonna

Leo ni leo ndivyo unavyoweza kusema! ni Mzizima Berby majira ya saa moja usiku katika uwanja wa Benjamin  Mkapa jijini Dar es Salaam mabingwa watetezi Simba watawakabirisha matajiri wa Chamazi Complex Timu ya Azam FC katika Mchezo wa Ligi ya NBC.

Simba ikitoka kushinda mabao 4-1 dhidi ya KMC katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora hivyo hivyo na Azam ikitoka kushindwa Mabao 4-1 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya maafande Ruvu Shooting mchezo wa leo unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Simba wakiwa na Kocha Mhispania  Pablo Franco,wapo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 21 wakiwa wamecheza mechi 9 huku Azam FC wakiwa nafasi ya 7 kwa Pointi 15 kwa kucheza mechi 10.

Leo ni leo nani ataanza na mwaka mpya kwa ushindi pamoja kuondoka na Pointi 3 na kuendelea kumfukuzia Yanga kileleni mwa Msimamo wa Ligi ya NBC akiwa na Pointi 29 baada ya jana kuufunga mwaka kwa ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya walima Arizeti Dodoma jiji katika uwanja wa Mkapa.

Baada ya mchezo wa leo wa Simba na Azam FC ligi itasimama na kupisha michuano ya mapinduzi ambayo inatarajia kuanza kesho katika uwanja wa Amani Zanzibar huku timu hizo zikitarajia kuanza safari kesho kwenda kushiriki michuano hiyo.