Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewasili katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuwapa pole wafiwa waliokuwa wamekusanyika ili kuwatambua ndugu na jamaa zao pia na majeruhi waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimpa pole moja ya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea juzi eneo la Msamvu Ndege wengi katika Wilaya ya Morogoro mjini baada ya kuwasili katika hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Mtafungwa baada ya kuwasili eneo la tukio ilipotokea ajali ya lori lililokuwa limebeba mafuata aina ya petrol na kusababisha vifo vya watu 62 na majeruhi 72.(Picha na Jeshi la Polisi)