Home Michezo TANZANITE YANYAKUWA KOMBE LA COSAFA U-20

TANZANITE YANYAKUWA KOMBE LA COSAFA U-20

0

************

NA EMMANUEL MBATILO

TIMU ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini baada ya kuitungua magoli mawili timu ya Taifa ya Zambia.

Magoli yalipatikana kupitia kwa nyota Opa Clement ambaye alipachika goli mnamo dakika ya 24 na baadae Protasia Mbunda alimalizia karamu ya mabao mawili katika dakika ya 87 na kufanikisha kubeba taji hilo.

bao kwa upande wa Tanzanite yalipachikwa na Opa Clement dakika ya 24 pamoja na Protasia Mbunda aliyefunga dakika ya 87 Uwanja wa Wolfson Port Elizabeth.

Tanzanite ambayo inaoongozwa na kocha mkuu Bakari Shime imeweza kuleta heshima kwa taifa na kuwajengea wanamichezo kujiamini na kulitangaza taifa ipasavyo katika ngazi ya soka na michezo kiujumla.