naibu meya wa manispaa yas Iringa Joseph lyata akizungumza na kikundi cha wafanyabiashara wa minadani (WAMMA) wakati wakusuluusha mgogoro uliokuwepo kati wa viongozi waliokuwepo na wanachama waliotuhumiwa kutafuna fedha
wanakikundi wa kikundi cha wafanyabiashara wa waminadani (WAMMA) wakimsikiliza naibu meya Joseph Lyata wakati wakusikiliza a kutatua mgogoro wao na viongozi waliokuwepo.
*************************************
NA RAYMOND MINJA IRINGA
NAIBU meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata ametoa siku tano kwa
kikundi cha wafanyabiashara wa minadani (WAMMA) kuitisha uchaguzi na
kuchaguzi wa viongozi wapya ili kuepusha migogoro isiyokuwa na lazima.
Uamuzi huo wa naibu meya umekuja mara bada ya viongozi wa kikundi
hicho kijiuzula nafasi zao jana na kuacha uongozi kwa viongozi wa
mpito kwa kile kinachodaiwa kuendesha kikundi hicho kwa ubabe na
kutafuna vedha za wanachama .
Akizungumza nma wanachama hao kwenye mkutano alioutisha ili kutafuta
suluhu na kuhudhuriwa na watendaji wa manispaa pamoja na madiwani wa
CCM lyata alisema kuwa mara baada ya kusikiliza pande zote mbili na
viongozi kuandika barua ya kujiuzuli ni vema kufanya uuchaguzi na
viongozi wapya ili kuendesha kikundi hivyo bila ya migogoro yoyote.
“Ndugu zangu sasa tumefikia sehemu nzuri tumefanya mazungumzo kwa
Amani bila hata ya kuwepo kwa polisi na viongozi wamekiri mapungufu
yao na katika hali ya kawaida hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu
na ha ta nyie wanachama muna mapungufu yenu hivyo basi ndani ya siku
tano tumekubaliana hapa tuitishe mkutano mkuu na tufanye uchaguzi wa
viongozi wetu mana hawa waliopo hawapo kisheria “ alisema lyata
Lyata alisema kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo ni watu muhimu sana
kwenye nchi hii na ndio maana mh Rais John Magufuli amekuwa
akiwatetea na kuwapigania wafanyabiashara wadogo hasa machinga na
ndio maana akatoa maelekezo kwa viongozi aliowateuwa kuwapigania
wafanyabiashara hao ili wasibughuthiwe na mtu yoyote .
“Ndugu zangu nyie ni watu muhimu sana mumekuwa mukifanya kazi nzuri na
ndio maana nchi yetu inasionga mbele kwani sote tunategemeana na ndio
maana leo tumekuja hapa pamoja na watendaji wa manispaa ili kufanya
kikundi hiki kisife bali kiendelea na badaye hata kuja kuwa benki kama
vikundi vingine vilivyo anza” alisema Lyata
Kwa upande wake diwani wa kata ya mshindo Ibrahimu Gwanda ambaye ndio
mlezi na msimamizi wa kikundi hicho aliwataka viongozi wa kikundi
hicho kuwa karibu na viongozi wa kata hiyo ili kuweza kutafuta suluhu
ya matatizo yao kuliko kusubiri mpaka kikundi kinataka kufa ndipo
wanapojitokeza .
“Ndugu zangu mimi nimeshanga sana mumekaa kimya mpaka mambo yanataka
kuharibika mimi ndio diwani wenu na ndio mumesajiliwa kwenye kata
yangu na hata kama kuna watendaji wangu hawawatendei haki basi pigeni
simu kwangu moja kwa moja namimi nitawasikiliza na kuwasaidia mana
mimi ndiye mwenye msiba basi tutalia wote’’ alisema Gwada
Gwada alisema kuwa atahakikisha kikundi hicho na vikundi vingine
vilivyo katika kata yake vinasimama imara na bila wanachama wake
kudhulumiwa fedha zao au kuyumba ili waweze kufanya kazi zao kwa faida
na mwisho wa siku kila mtu aweze kuneemeka na matunda ya jasho lake .