*************
NA MWAMVUA MWINYI,Morogoro
Mwenge wa uhuru, umekataa mradi wa maji uendelevu wake,katika kijiji cha Mautanga,kata ya Michenga,Ifakara mkoani Morogoro ,mradi ambao unaendeshwa na mamlaka ya maji safi na maji taka (IFUWASSA).
Ofisa TAKUKURU wilaya ameagizwa kwenda kufuatilia kwa kina kisha taarifa zipelekwe kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 ndani ya wiki mbili ,na taarifa hizo zipelekwe TAKUKURU Makao Makuu.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake hawajauridhia mradi huo ,kutokana na utofauti wa fedha baina ya mkoa na wilaya na kutopimwa kwa mabomba na kukiuka kipengele cha material test ambapo fedha ilishatengwa kiasi cha sh.laki sita.
“Tumebaini kuna utofauti wa taarifa kwenye mkataba,mkoa inaonyesha milioni 393.5 huku wilaya ikionyesha milioni 393 pekee kwahiyo hatuelewi tushike lipi na kina nani wapo sahihi na kwa lengo gani”
Mkongea alisisitiza,endapo itabainika kuna sintofahamu ,wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.