MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Dkt. Suleiman Misango (katikati), akifafanua jambo wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo viwanja vya Nyakabindi, Nanenane Simiyu.
Dkt, Misango na Meneja wa TRA Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Meneja Msaidizi Itifaki na Uhusiano Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Vicky Msina.
Dkt. Misamngo akizungumza huku ameshika mashine ya kutoa risiti za kielektroniki EFD, wakati alipotembelea banda la TRA.
…………………………………………….
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Dkt. Suleiman Misango ametembelea banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa kwenye viwanja vya Nayakabindi nje kidogo ya Maji wa Bariadi Mkoani Simiyu na kusema, ili kuhamasisha wananchi kulipa kodi ni lazima wapate elimu zaidi kwanini wanalipa kodi.
“Kodi ni mtu aweze kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa, lakini ni lazima aweze kujua zaidi kwanini analipa kodi, akishajua sababu za kulipa kodi kutakuwa na hamasa ya mtu huyo kulipa yeye mwenyewe bila kushurutishwa (voluntary compliance)na itapunguza vitu vingine vinavyoitwa Tax distortion….” Alisema Dkt,. Misango na kuongeza
“Kama wewe unatumia nguvu nyingi sana, unakwenda kwa mtu kudai kodi nayeye akakimbia, anaacha shughuli zake pale, na hiyo shughuli aliyokuwa anafanya kama angeweza kuzalisha kiwango fulani hatoweza kuzalisha na kunakuwa na distortion kwa siku hiyo, issue hapa ni kuongeza mapato na kupunguza tax distortion.” Alifafanua Mwenyekiti huyo wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania BoT.
Akizungumzia uwepo wa TRA kwenye maonesho ya Nanenane, Dkt. Misango alisema maonesho hayo ni fursa nzuri kwa Mamlaka hiyo kuwaelimisha wananchi kwanini wanatakiwa kulipa kodi na faida ya kodi hizo wanazolipa kwa mwananchi mwenyewe na taifa kwa ujumla.
“Lengo kuu wananchi wapate uelewa wa shughuli za TRA, na hii itawahamasha wanachi kuwa katika nafasi nzuri ya kuwajibika mojakwamoja kulipa mkodi na hapa mnaona kuna michoro mbalimbali inayoonyesha miradi mikubwa na midfogo inayotekelezwa na Serikali kutokana na kodi ambazo wananchi wanalipa.” Alifafanua.