Wananchi wakiwa katika banda la Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Wananchi wakiwa katika banda la Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mwandishi wetu,Babati.
Wambao wanaoishi katika maeneo ambayo yamekuwa yakivamiwa na tembo, wameshauri kutumia nyuki kudhibiti tembo lakini, pia kunufaika na biashara ya asali kutokana na nyuki hao.
Afisa Uhifadhi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), Julius Robinson ametoa wito huo, leo wakati akizungumza na wakulima, katika banda la taasisi hiyo, katika maonesho ya Nanenane kitaifa, viwanja vya Vyakabindi wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.
Robinson amesema,Nyuki wanafaida kubwa,kama wakitumiwa vizuri na wafugaji, hasa katika udhibiti wa tembo na kupata asali kwa takriban mwaka mzima.
“kutokana na umuhimu wa nyuki FCF tumekuwa na mradi wa kuwapa mizinga ya kibiashara wananchi wanaoishi wilayani Meatu, ambapo taasisi hii imewekeza katika shughuli za utalii wa picha na uwindaji kupitia kampuni ya Mwiba Holding na nyingine “alisema
Alisemaa hadi sasa mizinga zaidi ya 100 imetolewa kwa vikundi vya ufugaji nyuki, wilayani Meatu mkoa wa Simiyu na sasa vinapata asali lakini mazao yao hayavamiwi na Tembo.
Akizungumza katika banda hilo, Afisa nyuki wa wilaya ya Serengeti, Fares Mwacha alisema mizinga ambayo inatolewa na FCF ni rafiki kwa ufugaji wa nyuki na mfugaji anaweza kuvuna asali mwaka mzima bila nyuki kuhama katika eneo lake.
“hii mizinga ni ya kisasa na unaweza kuvuna asali bila kuuwa nyuki ama nyuki kuhama lakini, pia unaweza kuwatumia nyuki kuzuia wanyama kama Tembo kuvamia shamba lako”alisema
John Masunga mkazi wa Meatu kijiji cha Makao, anasema tangu wameanza kutumia mizinga hiyo, wamekuwa wakivuna asali lakini pia wanadhbiti Tembo, kutokana na kuweka mizinga pembezoni mwa mashamba yao.
Taasisi ya FCF kupitia kampuni zake imewekeza katika eneo la jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Makao na pori la akiba la Maswa, wilayani Meatu ambapo kwa mwaka licha ya kutoa misaada katika vikundi vya kijamii, imekuwa ikitoa zaidi ya sh 500 milioni kuchangia miradi ya maendeleo.