Home Mchanganyiko KWANDIKWA AWATAKA MTWARA KUONGEZA UZALISHAJI

KWANDIKWA AWATAKA MTWARA KUONGEZA UZALISHAJI

0

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bw, Gelasius Byakanwa akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kagua maendeleo ya ujenzi wa barabara na kiwanja cha ndege mkoani humo.

Muonekano wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50 ambayo ujenzi wake unaendelea.

Kazi ya ujenzi wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiendelea.

Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS), mkoa wa Mtwara Eng. Dotto John (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50, mkoani Mtwara (kushoto) ni mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw, Evod Mmanda na Afisa wa Wizara ya Ujenzi Bw, Boniface Myalla .

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akipata kahawa pamoja na wanakijiji wa Nanguruwe mkoani Mtwara ikiwa ni furaha yao kupata barabara ya lami katika kijiji hicho.

Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS), mkoa wa Mtwara Eng. Dotto John (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mtwara.

Kazi ya ujenzi wa njia ya kutua na kuruka ndege katika kiwanja cha ndege cha Mtwara ikiendelea, kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha ndege kubwa kutua katika kiwanja hicho.

…………………………………………………..

Wakazi wa mkoa wa Mtwara wametakiwa kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili waweze kutumia vizuri fursa za ujenzi wa miundombinu ya barabara, anga na bandari kujiimarisha kiuchumi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ukanda wa kusini mwa Tanzania unafunguka kimiundombinu katika nyanja za barabara za lami, bandari na usafiri wa anga hivyo kazi inayowakabili wananchi ni kuongeza uzalishaji.
Akizungumza na wanakijiji wa Nanguruwe mkoani humo mhe. Kwandikwa amesisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuweka fursa ya miundombinu bora katika kila kanda ili wananchi waitumie kukuza uchumi binafsi na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025.
“Tumejipanga kuhakikisha nyanja zote za usafiri zinaimarika katika ukanda huu wa kusini hivyo nawaomba zalisheni kwa wingi mazao ya chakula na biashara ili kufikia soko kwa haraka popote lilipo,” amesema mhe. Kwandikwa.
Aidha amemhakikishia mkuu wa mkoa wa Mtwara Bw, Gelasius Byakanwa kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha wilaya zote za mkoa wa Mtwara zinaunganishwa kwa barabara za lami katika kipindi kifupi ili kufikika kwa urahisi wakati wote na hivyo kuimarisha huduma za biashara.
Mhe. Kwandikwa yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50 na uwanja wa ndege wa Mtwara unaorefushwa kutoka mita 2258 hadi mita 2800 hali itakayowezesha ndege nyingi na zinazochukua abiria wengi kutumia uwanja huo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Agosti 5, 2019.