……………………
Na Mwandishi Wetu, PORT ELIZABETH
TIMU ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 8-0 dhidi ya Eswatini jioni ya leo Uwanja wa Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Mabao ya Tanzanite inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime anayesaidiwa na Edna Lema yamefungwa na Nahodha Enekia Kasonga mawili dakika za 24 na 74, Aisha Masaka matatu dakika za 39, 51 na 58, Irene Kisisa 41, Shamim Salum dakika ya 75 na Mabanza Gindulya dakika ya 87.

Mara baada ya mchezo, nyota wa Tanzanite, Diana Msemwa alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora hiyo ikiwa mara ya pili mfululizo.
Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Tanzania, baada ya Ijumaa kuichapa 2-0 Botswana Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth pia mabao ya Opa Clement dakika ya 38 na Klaotswe aliyejifunga dakika ya 48.
Tanzanite itateremka tena dimbani Jumanne kumenyana na Zambia kukamilisha mechi zake za Kundi B. Kundi A linaundwa na wenyeji, Afrika Kusini, Namibia, Msumbiji na Zimbabwe na michuano hiyo iliyoanza juzi, itafikia tamati Agosti 11 mjini Port Elizabeth.