Home Michezo MAN CITY YAICHAPA 5-4 LIVERPOOL KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO YA JAMII

MAN CITY YAICHAPA 5-4 LIVERPOOL KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO YA JAMII

0
Sergio Aguero (katikati kushoto) na David Silva (katikati kulia)  wakiinua Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Liverpool kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Wembley mjini London leo. Raheem Sterling alianza kuifungia Manchester City dakika ya 23 akimalizia pasi ya Silva, kabla ya Joel Matip kuisawazishia Liverpool dakika ya 77 akimalizia pasi ya beki Virgil van Dijk.
Kwenye mikwaju ya penalti, Xherdan Shaqiri, Adam Lallana, Alex Oxlade-Chamberlain na Mohamed Salah waliifungia Liverpool, wakati Georginio Wijnaldum alikosa na Ilkay Gundogan, Bernardo Silva, Phil Foden,Oleksandr Zinchenko na Gabriel Jesus waliifungia Man City PICHA ZAIDI SOMA HAPA