*************************
na makuzi bora ya watoto na kuwaimarishia ulinzi na usalama,kuimarisha uchumi wa kaya,masuala ya UKIMWI kwa vijana na afya ya uzazi, kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Shinyanga limefadhili kuanza kutengenezwa kwa mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mpango mkakati huo umeanza kutengenezwa leo Mei 24, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, kwa kuhusisha maofisa maendeleo, ustawi wa jamii, dawati la jinsia na watoto, wachumi, wanasheria, waratibu wa afya ya uzazi, maofisa elimu, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo washiriki hao wanatoka katika halmashauri zote sita za mkoa huo.
Akizungumza kwenye kikao hicho,Meneja wa Shirika hilo la ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram, alisema mwaka jana (2018) walishirikiana na serikali ya mkoa wa Shinyanga kuunda kamati ya mkoa ya ulinzi na usalama kwa watoto na wanawake, ambapo ilipewa mafunzo ya siku tatu na wizara ya afya kwa kushirikiana na ICS juu ya masuala ya MTAKUWWA, kwa ajili ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto.
Amesema baada ya kutolewa mafunzo hayo ndipo ikaazimiwa kutengenezwa mpango mkakati wa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kushughulikia masuala hayo ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto ili kufanikisha mpango wa Serikali (MTAKUWWA) wa kutokomeza ukatili huo kutoka asilimia 37 hadi asilimia 10 ifikapo 2022.
“Kikao cha leo ni cha kwanza ambacho tunatengeza mpango mkakati wa kutokomeza masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Shinyanga pamoja na kuunda timu ya wataalamu itakayo kwenda kuanza kazi ya kukamilisha utengenezaji wa mpango mkakati mara moja ili kutokomeza ukatili huo,”amesema Kudely.
“Mbali na kushirikiana na Serikali ya mkoa wa Shinyanga pia tumehusisha na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni SAVE THE CHILDREN, AMREF, JHPIEGO, TVMC, AGAPE, WORDVISSION, NA JSI ,kwa lengo la kuunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza masuala ya ukatili kwa wananawake na watoto mkoani hapa,”ameongeza.
Naye mgeni rasmi kwenye kikao hicho katibu tawala msaidizi utumishi na utawala mkoani Shinyanga Amos Machilika, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo, alisema mpango huo mkakati utaleta matokeo chanya ya kupungunza ukatili mkoani humo dhidi ya wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni.
Aidha amesema mkoa wa Shinyanga bado unaongoza kwa masuala ya ndoa za utotoni kwa asilimia 59,ikifuatiwa Tabora 58, na Dodoma 51, ambapo pia kwa mwaka jana kuanzia Julai hadi Disemba jumla ya matukio 31 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa.
Pia ametaja takwimu za mimba za utotoni mkoani Shinyanga kuwa ni asilimia 34 kwa mujibu wa takwimu za viashiria vya hali ya kiafya nchini (TDHS) ya Mwaka 2016, ikitanguliwa na Katavi 45, Tabora,43, Dodoma 39, na Mara 37, ambapo wastani wa kitaifa ni asilimia 27, huku kwa kipichi cha miaka mitatu jumla ya wanafunzi 351 walipewa ujauzito na kuacha masomo mkoani humo.
Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakiwasilisha mada akiwamo Afisa Ustawi wa Jamii Kahama Mji Ibrahimu Nuru, amesema ili kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto mkoani humo kuondoa kwanza tatizo la mila na desturi Kandamizi pamoja na kuimarisha uchumi wa kila Kaya.