Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Nnunduma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mwenge huo wa Uhuru leo umekimbizwa katika wilaya ya Kisarawe na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG-KISARAWE)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimzsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo wakati akitoa hotuba fupi ya kupokea mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo ukitokea Mafia Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe Bw Mtela Mwampamba.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimsikiliza Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Homboza wilayani Kisarawe ambapo mwenge wa Uhuru umekagua kituo hicho na kuridhika na ujenzi wake,
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimpongeza Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Homboza wilayani Kisarawe ambacho kimekamilika katikati ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Homboza wilayani Kisarawe ambacho kimekamilika huku Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo akishuhudia
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali na na wakimbiza mwenge wenzake wakikagua daraja la daraja la Kwa Konzo kata ya Msimbu wilayani Kisarawe
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Suleiman Jafo wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika daraja la Kwa Konzo Kata ya Msimbu wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mh.Zainab Vullu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimpongeza Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Kwa Konzo kata ya Kata ya Msimbu wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mh.Zainab Vullu.
……………………………………………………….