Wadau wa masuala ya Jinsia wakijadiliana na kupitia Kitini cha Mwongozo wa Masuala ya Jinsia na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kuufanyia majaribio ili uweze kusambazwa kwa wadau wote kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya, Kata hadi Taifa mapema jana mjini Morogoro.

……………………………………………..
Na mwandishi wetu Morogoro
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Grace Mwangwa amewataka wadau wa masuala ya Jinsia Nchini kuhakikisha wanatumia kitini cha mwongozo wa masuala ya jinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutokomeza vitendo vya ukatili kwa 50% ifikapo 2021/2022.
Bi. Mwanga aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati wadau wa masuala ya Jinsia walipokutana kupitia mwongozo huo kwa lengo la kuufanyia majaribio ili uweze kusambazwa kwa wadau wote kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya hadi Taifa ili uweze kutumika kutokomeza vitendo vya ukatili kama ilivyobainisha katika Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Aidha Bi. Mwangwa aliwataka wadau hao kutumia uelewa waliaoupata kuhuasu kitini hicho kusaidia Jamii kubaini na kukemea mila na desturi zenye madhara kwa jamii lakini pia kuwahakikisha kuwa Idara yake itaweka maboresho yaliyopendekezwa na wadau hao kabla ya kuwasilisha kitini hicho kwa hatua zaidi.
Bi. Mwangwa aliongeza kuwa kwa kipindi cha January – Disemba mwaka 2016 takwimu zinaonesha kuwa wanawake 307 walikumbana na ukatili wa vipigo na kuongeza kuwa idadi hiyo iliongezeka kwa matukio 43 zaidi na kufanya matukio hayo kufikia 350 kwa mwaka 2017.
Majaribio ya kitini hiki ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto wenye maeneo nane ya kimkakati na utekelezaji wake ulianza tangu mwaka 2017/18 na undelea kutekelezwa hadi ifikapo mwaka 2021/22.