……………………………………………………………………….
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya baadhi ya wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha na kuwa raia wema kwani Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.
IGP Sirro amesema hayo leo akiwa West Kilimanjaro wilaya Siha katika shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifunga mafunzo ya Kikosi Maalum cha kupambana na uhalifu mkubwa, mafunzo yaliyofanyika kwa muda wa wiki sita ambapo jumla ya wanafunzi 183 ambao ni askari wa Jeshi hilo wamehitimu.
Hata hivyo, IGP Sirro amesema kuwa, licha ya kwamba jamii imebadilika kwa kiasi kikubwa lakini wapo wasiotaka kubadilika na kutakiwa kubadilika.
Wakati huo huo IGP Sirro pia amezungumza na askari ambao ni wanafunzi wa kozi ya uongozi mdogo wa cheo cha Sajini kujifunza kwa weledi ili wawe viongozi bora na kuwatumikia wananchi.