Home Mchanganyiko RC MAHENGE AKERWA NA KASI NDOGO UJENZI WA DARAJA LA BAURA KONDOA

RC MAHENGE AKERWA NA KASI NDOGO UJENZI WA DARAJA LA BAURA KONDOA

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miondombinu katika Wilaya ya Kondoa alipokuwa akikagua daraja la Baura linalounganisha kata za Baura na Haubi daraja linalojengwa kwa gharama ya bilioni 5.4 na linatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi march 2021.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akikagua daraja la Baura linalounganisha kata za Baura na Haubi daraja linalojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.4 na linatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi march 2021.

Kaimu Meneja wa Wakala la barabara nchini TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Salome Kabunda  akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ya kukagua miondombinu ya barabara katika Wilaya ya Kondoa alipokuwa akikagua daraja la Baura linalounganisha kata za Baura na Haubi daraja linalojengwa kwa gharama ya bilioni 5.4 na linatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi march 2021.

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makota akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ya kukagua miondombinu ya barabara katika Wilaya ya Kondoa alipokuwa akikagua daraja la Baura linalounganisha kata za Baura na Haubi daraja linalojengwa kwa gharama ya bilioni 5.4 na linatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi march 2021.

Mhandisi mkazi anayesimamia mradi wa daraja la Baura, Mhandisi Alan Mpunga akitolea ufafanuzi jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa alipofika katika daraja hilo wakati wa ziara yake ya kukagua miondombinu ya barabara katika Wilaya ya Kondoa.

Meneja Mradi wa kampuni ya Mtwivila Traders Limited inayojenga daraja la Baura Mhandisi Derick Bwire akitolea ufafanuzi jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa alipofika katika daraja hilo wakati wa ziara yake ya kukagua miondombinu ya barabara katika Wilaya ya Kondoa.

………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Kondoa

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amekagua ujenzi wa daraja la Baura linalounganisha kata za Baura na Haubi Wilayani Kondoa Mkoani  Dodoma na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake ulitarajiwa kukamilika march 10, 2021 ili kuondoa kero ya mda mrefu ya wakazi wa kata hizo.

Pia ameagiza mradi huo kufanyiwa uchunguzi ni kwanini umetumia mda mrefu bila kukamilika licha ya kutengewa fedha nyingi na kuto kukamilika kwa wakati.

Dkt Mahenge amesema mradi huo ni wa mda mrefu lakini haujakamilika na wananchi waliotarajia kulitumia daraja hilo kuendelea kuteseka hasa katika kipindi hiki cha masika na mvua kubwa zikinyesha.

“Bado kazi iliyofanyika haijafikia matarajio Serikali ilitegemea daraja hili lenye zaidi ya shilingi bilioni tano lingekuwa tayari limeanza kutumika na wananchi kuepukana na shida ya miondombinu mibovu katika kipindi hiki cha mvua” amesema Dkt Mahenge.

Amesema haamini kama mvua ilikuwa kikwazo kikubwa kwa mkandarasi bali kasi ndogo ndio iliyosababisha daraja hilo kutokukalika kwa wakati kama ilivyotarajiwa wakati wa kuanza mradi huo wa daraja kubwa.

Amemtaka mkandarasi kuongeza kasi katika ujenzi wa daraja hilo ili mwishoni mwa mwezi march daraja liwe limekamilika na kwa kufuata viwango vinavyotakiwa ili lianze kutumika kwa kuwa litaweza kusaidia wananchi wengi wanaoishi katika kata hizo.

Aidha Dkt Mahenge akiwa katika kitongoji cha Hasu kata ya Haubi amemtaka Mratibu wa Wakala wa Bara bara za Mijini na Vijijini TARURA Mhandisi Lusako Kilembe kuingiza katika bajeti ya TARURA daraja linalounganisha Kitongoji cha Haubi na Msedi ambalo kwa mda mrefu imekuwa kero kwa wakazi wa vitongoji hivyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Salome Kabunda amesema mradi wa daraja hilo unahusisha ujenzi wa daraja mita 70.1 na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1.5 kwa pande zote ikigharimu bilioni 5.43 na sasa mradi upo asilimia 97 kukamilika kwake.

Amesema kuchelewa kwa mradi huo ni changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwamo kazi zilizojitokeza tofauti na ilivyotarajiwa na baadhi ya kipindi kuwa na mvua kubwa hasa zilizonyesha kuanzia novemba 2019 hadi April 2020 kuwa kubwa kuliko zilivyotarajiwa.

Nae Meneja mradi anayesimamia daraja hilo kutoka kampuni ya Mtwivila Traders Limited Mhandisi Derick Bwire ameahidi kutekeleza maagizo yote ikiwamo kumaliza ujenzi wa daraja hilo kwa mda aliopewa.