Home Mchanganyiko KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA MIRADI...

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA MIRADI YA TBC

0

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe. Stanslaus Nyongo (katikati mbele) ameongoza kamati hiyo leo Machi 13, 2021 kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linalojengwa Mikocheni jijni Dar es salaam kuboresha huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe. Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia mbele) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto mbele) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara leo Machi 13, 2021 kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linalojengwa Mikocheni jijni Dar es salaam kuboresha huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiwa katika maeneo mbalimbali wakati kamati hiyo ilipofanya ziara kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linalojengwa Mikocheni leo Machi 13, 2021 jijni Dar es salaam kuboresha huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt. Ayub Rioba (wa pili kulia) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara leo Machi 13, 2021 kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la studio za shirika hilo linalojengwa Mikocheni jijni Dar es salaam.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakikifurahia jambo wakiwa ndani ya studio za kurushia matangazo za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara leo Machi 13, 2021 kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la studio za shirika hilo linalojengwa Mikocheni jijni Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe. Stanslaus Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watangazaji wa Aridhio leo Machi 13, 2021 wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linalojengwa Mikocheni jijni Dar es salaam. Wa tatu kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa.

(Picha na Richard Mwamakafu-WHUSM, Dar es Salaam)

……………………………………………………………………………………..

Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe. Stanslaus Nyongo amesema kamati yake imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linalojengwa Mikocheni jijni Dar es salaam kuboresha huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Kamati hiyo imefanya ziara ya siku mbili ambayo ilianzia Dodoma Machi 12 na kuhitimishwa Machi 13, 2021 jijini Dar es salaam kwa kutembelea miradi iliyotekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mradi mwingine ni unaotekelezwa Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Dodoma ambao unaohusisha ukarabati wa jengo la studio na ununuzi wa mitambo na vifaa vya redio jamii.

“Nimeridhika na maendeleo ya ujenzi wa jingo la TBC 2 linalojengwa hapa Mikocheni, wajumbe wa kamati yangu wameridhika na ujenzi wa mradi huu unaolenga kuboresha huduma ya utangazaji na utoaji wa habari za ukweli na uhakika kwa wananchi” alisema Mhe. Nyongo.

Katika majumuisho ya ziara yao, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buyungu mkoani Kigoma Mhe. Aloyce Kamamba amesisitiza uongozi na watumishi wa shirika hilo kutunza majengo na kuwa na matumizi sahihi ya vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya televisheni na redio ya Taifa na vitumike kama vilivyokusudiwa.

“Muende vijijini walipo wananchi wengi na ndio shughuli nyingi za kiuchumi zinafanyika, mtumie vizuri vifaa mlivyopata, mjikite zaidi na shughuli zinazofanywa na vijana pamoja na kuhakikisha mikoa ya mipakani usikivu wa redio uwe wa uhakika ili kuwapa wananchi wote haki yao ya msingi ya kupata taarifa juu ya shughuli zinazotekelezwa na Serikali yao” alisema Mhe. Kamamba.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameishukuru kamati hiyo kwa kutembelea miradi hiyo na kusisitiza Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo na imepokea maoni na ushauri waliotoa kwa TBC hatua inayoifanya Shirika hilo kuwa bora zaidi katika kuwapatia Watanzania haki yao ya Kikatiba ya kupata taarifa.

“TBC inaendelea kuimarika, kumekuwa na ubunifu na vionjo vizuri kama Aridhio ambayo inapendwa sana nchini na imetoka kwenye mfumo wa analojia na sasa ipo kwenye mfumo wa kidijiti hatua inayofanya kuwafikia watu wengi na rika zote” alisema Mhe. Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema Wizara yake kama nguvu laini (soft power) inaendelea kuwa na mashirikiano kati Tanzania Bara na Visiwani katika sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na kamati hiyo ya Bunge na kuyafanyia kazi maoni yao waliyoyatoa kwa shirika hatua inayosaidia kuboresha maudhui ya Televisheni na Redio ya Taifa.