Na Mwandishi Wetu, Arusha
MKAZI wa Unga Ltd jijini Arusha, Euralia Matai, ameiomba Serikali kuingilia kati kutatua changamoto ya mgogoro wa ardhi inayomkabili, akieleza kuwa suala hilo linahusisha migogoro ya umiliki na uvamizi wa viwanja.
Matai amewasilisha malalamiko yake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Sheria mkoani Arusha, Novemba 24, 2026, akitumia fursa hiyo kueleza changamoto zinazohitaji msaada wa kisheria na kuomba hatua za Serikali zitakazowezesha kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro huo.
Uzinduzi wa kliniki hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kusogeza huduma za msaada wa kisheria karibu na wananchi ili kuwapa fursa ya kupata ushauri na msaada katika kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu masuala ya kisheria.
