…………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kiman’ta amemshukuru Rais wa jamuhuri ya Muunganano wa Tanzania John Magufuli kwa kutoa ndege ya serikali kubeba mwili wa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega kuelekea kwenye maziko jijini mwanza.
Akitoa ratiba ya kuaaga mwili kwa waandishi wa habari Kimanta alisema kuwa Rais Magufuli ameonyesha kuthamini utendaji wake wa kazi na ameonyesha heshima kubwa kwa kiongozi mwenzao.
Alisema ratiba ya kuaga na kuelekea kwenye maziko itaanza kesho ijumaa asubuhi ambapo i majira ya 7:50 mwili utachukuliwa katika chumba Cha kuhifadhia maiti nakupelekwa nyumbani kwake na baada hapo wataondoka nyumbani na kwenda katika kanisa la mtakatifu Theresa kwaajili ya misa.
Alisema misa itaanza saa mbili kamili asubuhi hadi saa tatu na baada ya hapo wataondoka kuelekea uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya hutuba ya mkuu wa mkoa na Salamu mbalimbali za rambirambi ambazo zitaambatana na kuaga mwili wa marehemu na zoezi hilo litaanza saa 9:25 asubuhi hadi saa 1:30 mchana na baada ya hapo maandalizi ya kwenda uwanja wa ndege wa Arusha yataanzaa na wanatarajia kuondoka majira ya saa 3: 00 alasiri kwenda mwanza.
Alifafanua kuwa baada ya kufika jijini Mwanza mwili utapelekwa nyumbani kwake Buswalo ambapo utalala hadi asubuhi ambapo majirani watapata wasaa wa kuaga na baada ya hapo wataelekea Wilaya ya Sengerema Katika Cha Ngoma ambapo ndiko alipozaliwa kwajili ya ibada na maziko ambayo yatafanyika alasiri jumamosi.