Home Mchanganyiko MWENYEKITI CCM DODOMA AKIWA NA KAMATI YA SIASA YA MKOA WASHUHUDIA AHADI...

MWENYEKITI CCM DODOMA AKIWA NA KAMATI YA SIASA YA MKOA WASHUHUDIA AHADI YA RAIS MAGUFULI IKITIMIA KWA WAKAZI WA MBANDE.

0

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akitoa maelezo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara inayounganisha mji wa Mpwapwa ambapo ameongozana na  Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma  kukagua na kujione Miradi mbalimbali  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri,alipotembelea na kukagua ujenzi wa  barabara inayounganisha mji wa Mpwapwa ambapo ameongozana na  Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma  kukagua na kujione Miradi mbalimbali  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

 

Muonekano wa barabara inayojengwa

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk. Suleiman Serera,akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akiwa ameongoza na Kamati ya Siasa ya Mkoa kabla ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM .

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akiwa ameongoza na Kamati ya Siasa ya Mkoa akiwaonyesha watumishi wa wilaya Kongwa Ilani ya CCM kabla ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM .

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akitoa maelezo wakati wa kukagua mradi wa kisima cha Maji kilichopo wilayani Kongwa ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja DUWASA Kongwa Bw.Amran Gama  mara baada ya kukagua mradi wa kisima cha Maji kilichopo wilayani Kongwa ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.Suleimani Serera pamoja na  Kamati ya Siasa ya Mkoa wakimsikiliza Meneja wa DUWASA Kongwa mara baada ya kutembelea  miradi  wa Maji  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akipata taarifa ya ujenzi wa Chuo cha Veta Kongwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ujenzi VETA Kongwa Bi.Paskalina Duwe wakati alipotembelea ujenzi huo  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

 

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akipata taarifa ya ujenzi wa Chuo cha Veta Kongwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ujenzi VETA Kongwa Bi.Paskalina Duwe wakati alipotembelea ujenzi huo  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akitoa maelezo mara baada ya kukagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ndugai inayojengwa  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.Suleimani Serera mara baada ya kukagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ndugai inayojengwa  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Muonekano wa ujenzi wa Darasa la Shule ya Msingi Ndugai ukiendelea.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.Suleimani Serera walipotembelea  na kujionea ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Segeli, aliyoitoa Rais Dk. John Magufuli kwa wakazi wa Mbande, Wilaya ya Kongwa, imetimia baada ya ujenzi wake kukamilika ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akipokea taarifa ya ujenzi kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk. Thomas Samweli alipotembelea na kujionea ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Segeli, aliyoitoa Rais Dk. John Magufuli kwa wakazi wa Mbande, Wilaya ya Kongwa, imetimia baada ya ujenzi wake kukamilika ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akizungumza mara baada ya kukagua na kujionea ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Segeli, aliyoitoa Rais Dk. John Magufuli kwa wakazi wa Mbande, Wilaya ya Kongwa, imetimia baada ya ujenzi wake kukamilika ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Moja ya jengo lililopo katika  Kituo cha Afya Segeli, Mbande, Wilaya ya Kongwa.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akimsikiliza Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw.Elias Binamungu  alipofanya ziara ya kutembelea ranchi hiyo  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mwenyekiti wa CCM Dodoma,Godwin Mkanwa akizungumza mara baada ya kutembelea Ranchi ya Kongwa  ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

   

Ng’ombe wakiwa katika Ranchi ya Taifa iliyopo Kongwa

………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Kongwa

Katika kuelekea Siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Mwenyekiti CCM Dodoma,Godwin Mkanwa wameshuhudia ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Segeli, aliyoitoa Rais Dk. John Magufuli kwa wakazi wa Mbande, Wilaya ya Kongwa, imetimia baada ya ujenzi wake kukamilika kwa gharama ya sh. milioni 400.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa CCM Bw. Mkanwa, amesema kuwa  Rais Dk. Magufuli akiahidi anatenda kwa vitendo.

Mkanwa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya Segeli kitakuwa mkombozi kwa wakazi wa Mbande na watumiaji wa barabara kuu ya Dodoma-Dar es Salaam.

“Nimeshangazwa na ujenzi wa kituo hiki cha afya, nakumbuka wananchi wa Mbande walimsimamisha Rais Dk. Magufuli na kumuomba awajengee kituo cha afya. Kimejengwa kwa haraka na wananchi wa maeneo haya na jirani watanufaika,” amesema Mkanwa

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk. Suleima Serera, amesema kuwa wananchi wanahitaji huduma za msingi ikiwemo afya na ndio sababu Rais Dk. Magufuli, ametimiza ahadi yake.

Dk.Serera amesema kuwa wao kama wilaya watasimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo kama ambavyo dira ya maendeleo ya taifa na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inavyoelekeza.

Awali Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk. Thomas Samweli, amesema kuwa kituo hicho kimejengwa ikiwa ni ahadi ya Rais Dk. Magufuli aliyoitoa kwa wakazi wa Mbande ambapo alitoa sh. milioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Dk.Samweli amesema kuwa kituo hicho cha afya kinahusisha jengo la wagonjwa wa nje, jengo la wajawazito, upasuaji na jengo la kufulia nguo za wagonjwa.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kongwa, Zubeir White, amesema kuwa ujenzi huo umefanyika kwa kiwango kinachostahili na wataendelea kusimamia miradi ya serikali itekelezwe kama inavyopaswa.