NA DENIS MLOWE IRINGA 

MASHINDANO ya Kombe la Ritta Kabati 2026 yamezinduliwa rasmi katika Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, na Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Dr. Ritta Kabati, Novemba na kufanyaka atika Uwanja wa Kihesa Mgagao, uliopo Kata ya Ng’uruhe.

Katika uzinduzi huo, timu 12 kutoka Tarafa ya Kilolo zimekabidhiwa vifaa vya michezo, huku timu 12 za ukanda wa chini zikitarajiwa kukabidhiwa vifaa hivyo leo kwa ajili ya kuanza kwa mashindano katika tarafa za Mazombe na Mahenge.

Mashindano hayo yameanza kwa mchezo wa ufunguzi uliowakutanisha Wangama FC na Kihesa Mgagao FC, ambapo Wangama FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mbunge Kabati amewahimiza vijana kutumia mashindano hayo kama fursa ya kukuza na kuendeleza vipaji vyao vya michezo, pamoja na kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao.

Aidha, amewataka vijana kutumia mashindano hayo kuhamasishana kuunda vikundi vya kiuchumi ili kunufaika na fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri pamoja na mikopo kupitia Wizara ya Vijana.

Dr. Kabati amesisitiza umuhimu wa nidhamu, umoja na kuheshimiana kwa vijana na timu zote zitakazoshiriki mashindano hayo, akieleza kuwa michezo ni jukwaa muhimu la kujenga vijana wenye afya, vipaji, maadili na uwezo wa kujiletea maendeleo.

Mashindano ya Ritta Kabati Cup 2026 yanatarajiwa kwauunganisha vijana wa Kilolo kupitia michezo, vipaji na fursa za maendeleo.