Mawakili wa Serikali, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameshiriki mafunzo kuhusu miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sketa binafsi (PPP).
Mafunzo yameratibiwa na kuendeshwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP – Center) na yamefanyika katika ukumbi wa PPP-Center Mtumba, jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2026.
Aidha, Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha Mawakili wa Serikali kupata uelewa wa kina wa dhana ya ubia, kutambua mifumo ya kisheria na kitaasisi inayosimamia utekelezaji wa miradi ya PPP.

