Wekundu wa Msimbazi Simba SC meendelea kuwa ya moto baada ya kushinda mchezo wake wake wa tisa mfululizo msimu huu ikizidi kujikita juu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote, ikiichapa Fountain Gate kwa bao 1-0.

Bao la dakika ya 33 kipindi cha kwanza likifungwa na beki na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Rushine De Reuck, likatosha kuihakikishia Simba ushindi huo, akifunga kwa kichwa wakati akitumia mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Nathaniel Chilambo.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 27 ikiendelea kuwa juu ya msimamo wa ligi ikiwaangalia kwa chini Yanga waliopo nafasi ya pili na pointi zao 22.