
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu umma kuwa umefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya kwanza, Manqoba Mngqithi.
Vile vile, Uongozi wa Young Africans Sports Club umesitisha mkataba na Kocha wa Viungo wa timu ya kwanza, Chyna Mokaila.
Uongozi unawashukuru Watendaji hawa kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri kwenye majukumu yao mapya.
Tayari mchakato wa haraka wa kumpata Kocha Mkuu mpya umeanza na unatarajia kukamilika hivi karibuni.
