Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamelazimishwa sare na TRA United katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga SC kubaki na pointi 19 baada ya kucheza michezo nane, huku wapinzani wao wa jadi, Simba SC, wakiendelea kuongoza ligi kwa pointi 24 baada ya kucheza michezo nane.
Kwa upande wa TRA United, matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kufikisha pointi saba baada ya kucheza michezo nane.
