Na Mwandishi wetu, Babati

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Regina Ndege Utumishi na Utawala Bora, Regina Ndege ameongoza uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 700 na utunzaji wa mazingira inayoratibiwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Regina ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Manyara ameongoza uzinduzi huo mjini Babati kwa kampeni ya upandaji miti 700 kwa kupanda miti 250 hospitalini hapo.

Kampeni hiyo inayoongozwa na mganga mfawidhi wa hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Yesige Mutajwaa.

Kampeni hiyo imepewa jina la Utumishi Pamoja na Kutunza Mazingira”* inalenga kupanda miti 700 na katika uzinduzi ikipandwa miti 250.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Naibu Regina amesisitiza miti iliyopandwa kutunzwa vizuri ili ikue na kuleta manufaa ya mazingira.

Hata hivyo, amewatoa hofu uongozi wa hospitali hiyo kwa changamoto ya uhaba wa watumishi, kwani Serikali inatarajia kutoa ajira.

“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kutoa ajira 45,000 na changamoto ya watumishi itatatuliwa,” amesema Naibu Waziri Regina..

Pia, Naibu Waziri Regina ametoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa watoto na wanawake wazazi waliojifungua na waliolazwa katika hospitali hiyo.