Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi wa wafugaji kutoka kata 40 za Wilaya ya Kilosa katika kikao cha pamoja cha kuweka mikakati ya kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Madiwani, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wakuu wa Idara, wataalamu mbalimbali na viongozi wa dini.