Tarehe 19 Oktoba 2026, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Caesar C. Waitara, alitembelea makazi ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Hifikepunye Pohamba, jijini Windhoek, kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha mke wake mpendwa, Marehemu Mama Penehupifo Pohamba, kilichotokea tarehe 17 Oktoba 2026.

Balozi Waitara aliwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akieleza masikitiko na mshikamano wa Tanzania na Namibia katika kipindi hiki cha maombolezo.