*Asema Serikali itaendelea kutatua changamoto za kiuwekezaji ili kuweka mazingira mazuri ya biashara;

*Asifu hatua ya ALAF kujenga Chuo cha ufundi kusaidia vijana kupata ujuzi mbali mbali 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa mwekezaji kutoka kiwanda cha mabati cha ALAF ambae ni Mtendaji Mkuu Bwana BIbhu Nanda kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kiuwekezaji na nia Yao ya kuwekeza kwenye Chuo cha ufundi hapa nchini 

Mhe Kapinga amesema Serikali itaendelea kutatua changamoto za kiuwekezaji ili kuweka mazingira mazuri ya biashara na kuongeza kuwa soko la mabati linafanya vizuri kwenye sekta ya biashara.

Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Mtendaji Mkuu wa ALAF Bibhu Nanda amesema ALAF imekusudia kufungua chuo cha ufundi stadi eneo la kisongo Arusha kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana kujifunza ujenzi na uezekaji wa Nyumba 

ALAF ni miongoni mwa wawekezaji Wakubwa hapa nchini ambao wanatarajia kuongeza uwekezaji zaidi hapa nchi ili kuongeza mauzo ya bidhaa hapa nchini na kuongeza kuwa miaka mitano ijayo itakuwa imewekeza Kiasi cha Bilioni 25.