Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, akiwa mgeni rasmi katika hafla maalum ya kumpokea Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Ndg. Kisena Mabuba, aliyeteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni, na kumuaga Mkurugenzi aliyehudumu katika wilaya hiyo, Bi. Bertice Mwinuka, aliyeteuliwa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mamboya, ikiambatana na chakula cha usiku na utoaji wa zawadi mbalimbali za shukrani na kumbukumbu.

