Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, akiwahudumia wateja na kuwaeleza manufaa ya programu ya PRIS na Puma Elite Card katika kituo cha Puma Airport Service Station. Kupitia huduma hizi, Puma Energy inalenga kuongeza thamani kwa wateja kwa kuwawezesha kupata zawadi kupitia manunuzi ya bidhaa za Puma, pamoja na kurahisisha usimamizi wa matumizi ya mafuta. Hatua hii ni sehemu ya dhamira ya kampuni ya kuwaweka wateja mbele na kuendelea kuboresha uzoefu wao wanapopata huduma za Puma Energy. Zoezi hilo limefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja
…………
Dar es Salaam-Tanzania, Oktoba 9, 2026:
Kampuni ya Puma Energy Tanzania inaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia programu yake ya uaminifu kwa wateja ya PRIS na kadi ya malipo ya Puma Elite Card, kupitia zoezi maalumu la kuwashirikisha wateja katika kituo cha mafuta cha Puma Airport Service Station. Zoezi hilo linalenga kuwapa wateja uelewa zaidi kuhusu namna wanavyoweza kupata zawadi, kurahisisha malipo ya mafuta na kudhibiti matumizi yao kwa urahisi zaidi.
Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za kampuni za kuongeza uelewa kuhusu huduma hizi na kuwahamasisha wateja kuzitumia, huku likiwapa fursa ya kufahamu namna zinavyoweza kuongeza thamani na kurahisisha matumizi yao ya kila siku wanapopata huduma katika vituo vya Puma Energy.
Kupitia PRIS, programu ya kidijitali ya Puma Energy inayowawezesha wateja kukusanya pointi na kupata zawadi, wateja hupata pointi wanaponunua bidhaa zinazostahili, zikiwemo mafuta, vilainishi vya injini, gesi na bidhaa zingine katika maduka ya Shop Express. Pointi hizo zinaweza kukombolewa kwa zawadi mbalimbali zinazopatikana kupitia programu hiyo, hivyo kuwawezesha wateja kupata manufaa zaidi kutokana na manunuzi yao ya kawaida.
Mbali na PRIS, Puma Energy pia inatoa Puma Elite Card, kadi ya malipo ya mafuta inayowawezesha watu binafsi, familia na biashara kudhibiti matumizi ya mafuta kwa urahisi zaidi. Wateja huweka fedha kwenye kadi hiyo na kuzitumia kununua bidhaa zinazostahili, zikiwemo mafuta, vilainishi vya injini na gesi. Kadi hiyo inakubalika katika vituo vya Puma na vituo washirika zaidi ya 80 nchini Tanzania.
Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, alisema kampuni inaendelea kutafuta njia za kuongeza thamani ya huduma zake kwa wateja na kuimarisha uhusiano wao na chapa ya Puma.
“Wateja wetu ni kiini cha biashara yetu, na tunaendelea kutafuta njia za kufanya uzoefu wao wanapopata huduma za Puma uwe bora zaidi, wenye manufaa na unaowapa urahisi. Kupitia PRIS, wateja wanaweza kupata zawadi kutokana na manunuzi yanayostahili, huku Puma Elite Card ikiwawezesha kusimamia matumizi yao ya mafuta kwa urahisi. Kwa kuwaletea huduma hizi karibu zaidi, tunalenga kuwasaidia wateja wengi kuelewa manufaa yake na namna wanavyoweza kuyatumia,” alisema Bi. Fatma.
Aliongeza kuwa mahitaji na matarajio ya wateja yanaendelea kubadilika, hivyo ni muhimu kwa kampuni kutoa huduma zinazoleta urahisi, ubunifu na manufaa yanayoonekana katika maisha yao ya kila siku.
“Tunataka kila mteja anapohusiana na Puma apate manufaa yanayoeleweka. Iwe ni kukusanya pointi na kupata zawadi kupitia PRIS au kusimamia matumizi ya mafuta kupitia Elite Card, lengo letu ni kutoa suluhisho linalokidhi mahitaji ya wateja. Kupitia zoezi hili, tunapata nafasi ya kukutana na wateja moja kwa moja, kujibu maswali yao na kuwaelekeza namna huduma hizi zinavyofanya kazi,” alisema.
Katika kituo cha Puma Airport Service Station, wateja watapata fursa ya kuzungumza na wawakilishi wa Puma Energy, kujifunza zaidi kuhusu huduma hizo mbili na kufahamu namna ya kunufaika nazo. Zoezi hilo linalenga kuongeza uelewa na matumizi ya huduma hizo, huku likiimarisha uhusiano kati ya kampuni na wateja wake.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Sheria na Mahusiano wa Kampuni wa Puma Energy Tanzania, Emmanuel Bakilana, alisema kutoa huduma zinazokidhi mahitaji mbalimbali ya wateja ni muhimu katika kujenga uhusiano wa kudumu na kuimarisha imani yao kwa kampuni.
“Mahitaji ya wateja yanatofautiana, na sisi tunalenga kutoa huduma zinazozingatia mahitaji hayo. Kupitia PRIS, wateja wanapata fursa ya kukusanya na kukomboa pointi za zawadi, huku Elite Card ikiwawezesha kufanya malipo kwa urahisi na kudhibiti matumizi ya mafuta. Kwa kuongeza uelewa kuhusu huduma hizi, tunataka kuwasaidia wateja kufanya maamuzi sahihi kuhusu huduma zinazowafaa zaidi,” alisema Bakilana.
Alisema Puma Energy itaendelea kuimarisha mawasiliano na wateja katika mtandao wake wa vituo kwa kuhakikisha taarifa kuhusu bidhaa na huduma zake zinapatikana kwa urahisi, ili wateja waweze kuelewa na kunufaika zaidi nazo.
Zoezi hilo linafanyika wakati Puma Energy Tanzania ikiungana na wadau wengine kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya mwaka 2026, kipindi kinachotoa nafasi ya kuwathamini wateja na kuonesha hatua zinazochukuliwa kuboresha uzoefu wao wanapopata huduma. Hata hivyo, juhudi za kampuni katika kuboresha huduma na kuongeza thamani kwa wateja zinaendelea mwaka mzima kupitia ubunifu na suluhisho zinazorahisisha upatikanaji wa huduma zake.
Tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania mwezi Mei 2026, PRIS imeongeza fursa ya kidijitali inayowawezesha wateja kukusanya na kukomboa pointi za zawadi, sambamba na huduma nyingine za Puma Energy kama Elite Card. Huduma hizi zinakidhi mahitaji tofauti ya wateja: PRIS huwapa fursa ya kupata zawadi kutokana na manunuzi yanayostahili, huku Elite Card ikiwawezesha kuweka fedha mapema na kudhibiti matumizi yao yanayohusiana na ununuzi wa mafuta.
Kupitia zoezi hilo katika kituo cha Puma Airport Service Station, kampuni inalenga kuwafikia wateja wengi zaidi, kuwaonesha namna huduma hizo zinavyofanya kazi na kuwahamasisha kuzitumia ili kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia mtandao wa vituo vya Puma Energy.
Kampuni ya Puma Energy inaendelea kujikita katika kutoa huduma zinazoongeza urahisi, manufaa na thamani kwa wateja, huku ikihakikisha kuwa kila wanapohusiana na kampuni wanapata uzoefu bora zaidi.

