Serikali ya Tanzania imetoa wito kwa taasisi za fedha na wawekezaji kuangalia kwa karibu fursa zinazoibuka kutokana na Sekta ya Uchumi wa Bluu ili kuchangia maendeleo endelevu ya nchi.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati akizindua rasmi mpango wa Biashara Endelevu za Uchumi wa Buluu nchini Tanzania (StawiBluu).
Uzinduzi huo umefanyika kando ya Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizindua StawiBluu hiyo Dkt. Kazi alisema kuwa ukuaji wa uchumi, maendeleo ya sekta binafsi na uendelevu wa mazingira vinaweza na lazima viende sambamba katika Uchumi wa Buluu wa Tanzania.
Aliwahimiza washirika wa maendeleo kuendelea kuunga mkono ushirikiano unaoimarisha taasisi za kitaifa, kujenga uwezo wa ndani na kuunda mifumo ya kudumu kwa ajili ya maendeleo ya biashara na uwekezaji.
“Mustakabali wa Uchumi wa Bluu wa Tanzania hautaamuliwa na ukubwa wa maliasili zetu pekee bali utaamuliwa na uwezo wetu wa kubuni, kuwekeza, kujenga biashara zenye ushindani na kusimamia rasilimali hizo kwa uendelevu,” alisema Dkt. Kazi.
Alieleza kuwa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 inasisitiza umuhimu wa mazingira rafiki ya uwekezaji, ubunifu, ujasiriamali na sekta binafsi imara kama vichocheo muhimu vya mabadiliko.
Halikadhalika, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Dira hiyo inatambua uchumi wa buluu kuwa miongoni mwa sekta zenye uwezo mkubwa wa kuchangia katika maendeleo ya Tanzania.
Alisema mwelekeo huu unaungwa mkono na Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2024 pamoja na Mkakati wake wa Utekelezaji wa mwaka 2024–2034, ambavyo vinaweka mfumo wa maendeleo yaliyoratibiwa na endelevu ya shughuli za Uchumi wa Buluu katika Tanzania Bara.
“Mifumo hii inaonesha kuwa Tanzania inavuka hatua ya kutambua tu uwezo uliopo katika Uchumi wa Buluu, sasa tunajikita katika kuugeuza uwezo huo kuwa utekelezaji, uwekezaji na matokeo yanayopimika. Katika muktadha huu, mpango wa StawiBluu unakuwa na umuhimu wa kipekee.,” alisisitiza.
Hivyo, alisema kupitia utekelezaji wa StawiBluu, unatarajiwa kusaidia biashara zinazozalisha ajira na thamani ya kiuchumi huku kukiwa tija ya muda mrefu ya bahari na mifumo ikolojia ya pwani.