Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elisha Suku, amefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini , Mhe. Nicole Providoli, tarehe 7 Oktoba 2026, jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ajenda za kimataifa, ikiwemo sheria za kimataifa, pamoja na fursa na mipango mbalimbali yenye maslahi ya pamoja kwa pande zote mbili.

