Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) ameitaka Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kufanya marekebisho muhimu ya mradi wa maji wilayani Hanang’ baada ya kubainika kasoro za kitaalam ambazo lazima zifanyike katika kuhakikisha uendelevu wa mradi.
Mhe. Kundo amefanya uamuzi huo tarehe 7 Oktoba 2026 ambapo alitakiwa kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Kinyamburi.
