🟠Hii ni baada ya bei kushuka kwa miezi mitatu mfululizo
🟠Serikali yaweka mkazo uhakika wa mafuta, uhimilivu wa bei nchini
Na Mwandishi Wetu  Â
Serikali imesema inaweka mkazo katika kuhakikisha bidhaa za mafuta zinaendelea kupatikana nchini kwa uhakika, na kwa bei himilivu, licha ya mabadiliko ya bei katika soko la dunia yanayoendelea kuathiri bei za ndani.
Serikali imechukua hatua hizo kutokana na mwenendo wa bei za mafuta nchini kuendelea kuathiriwa na mgogoro wa kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati, ambako Tanzania hununua sehemu kubwa ya bidhaa zake za mafuta, ambao uliibuka upya na kuathiri uzalishaji, upatikanaji na usafirishaji wa mafuta duniani.Hali hiyo ilisababisha kupanda kwa bei za bidhaa za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia.
Kutokana na mwenendo huo, bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini kwa mwezi Oktoba 2026 zimeongezeka ikilinganishwa na mwezi Septemba 2026. Bei zimepanda baada ya kushuka kwa miezi mitatu mfululizo.
EWURA, kama ilivyo wajibu wake, imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli zitakazotumika nchini kuanzia Jumatano, tarehe 7 Oktoba 2026, saa 6:01 usiku.
Kwa mwezi Oktoba 2026, katika mkoa wa Dar es Salaam, bei kikomo ya rejareja ni Shilingi 4,057 kwa lita ya petroli, Shilingi 4,086 kwa lita ya dizeli na Shilingi 4,067 kwa lita ya mafuta ya taa.
Kwa Tanga, bei kikomo ya rejareja ni Shilingi 4,123 kwa lita ya petroli, Shilingi 4,152 kwa lita ya dizeli na Shilingi 4,133 kwa lita ya mafuta ya taa.
Na kwa Mtwara, bei kikomo ya rejareja ni Shilingi 4,170 kwa lita ya petroli, Shilingi 4,199 kwa lita ya dizeli na Shilingi 4,180 kwa lita ya mafuta ya taa.Â
Taarifa hiyo iliyotolewa imewakumbusha wananchi kuchukua risiti baada ya kununua ya mafuta kwenye vituo ili kuwa na ushahidi wa ununuzi huo.Â
