Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judith Kapinga amekabidhi kilo 1,000 za mbegu za kahawa kwa AMCOS 20 na kikundi kimoja ili kuzalisha vitalu vya miche ya kahawa ili kuweza kuzalisha miche milioni 3.5 na kuendeleza jitihada za kuzalisha kahawa Wilayani humo.

Amekabidhi mbegu hizo Oktoba 07,2026 wakati wa Ziara yake alipotembelea Halmashauri ya Mbinga iliyopo katika Jimbo hilo ambapo amesema amesema uchumi wa Halmashauri hiyo ni kilimo cha kahawa kwani msimu uliopita halmashauri hiyo imezalisha tani elfu 18 na kwa msimu huu imepanga kuzalisha tani 19 ambapo mpaka sasa imevuka malengo hayo kabla ya msimu kuisha.

Waziri Kapinga ameongeza kuwa utoaji wa mbegu hizo ni kuchagiza uzalishaji wa kahawa kwa wingi ili kuchochea uchumi kwa wananchi wa Mbinga pamoja na upatikanaji wa mapato kwa halmashauri.