Na Jeshi la Polisi Dodoma 
Wanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Franco Badian iliyopo Mpwapwa mkoani Dodoma, wametakiwa kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa ama kukutana navyo ili hatua za kukomesha vitendo hivyo zichukuliwe.
Akitoa elimu hiyo Oktoba 6,2026 Mkaguzi Kata wa Kata ya Lumuma, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Mollel, amesema jamii inayowajibu wa kuwaelimisha watoto hususani wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kujiepusha na vitendo vya mmomonyoko wa maadili ambao wakati mwingine vinachangia kuharibu ndoto za wanafunzi na kutifikia malengo yao.
Mkaguzi Mollel, amesema katika Kata ya Lumuma jamii imeendelea kuwa na uelewa kuhusu maana ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto, hatua za kuchukua ikiwemo kufuatilia mienendo ya watoto wao wawapo nyumbani, shuleni na hata maeneo mengine ili kujenga jamii iliyobora yenye kizazi chenye maadili na kinacho heshimu wengine.