Wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania wakiongozwa na Afisa Mtendaji wa Benki hiyo, Jaffari Matundu, wakishiriki matembezi ya huduma kwa wateja 2026 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki hiyo yenye kaulimbiu “The Extra Mile” na kuonesha dhamira ya Benki ya kuwaweka wateja mbele.
Wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania wakishiriki matembezi ya huduma kwa wateja 2026 jijini Dar es Salaam, yenye kaulimbiu “The Extra Mile”.
Afisa Mtendaji wa Exim Bank Tanzania, Jaffari Matundu, akizungumza na wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 2026. Alisisitiza umuhimu wa kwenda hatua ya ziada katika kuwahudumia wateja na kuhakikisha kila mwingiliano unaleta thamani kwao.
Afisa Mtendaji wa Exim Bank Tanzania, Jaffari Matundu, akikata keki pamoja na baadhi ya wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 2026. Wiki hiyo yenye kaulimbiu “The Extra Mile” inalenga kuimarisha dhamira ya Benki ya kutoa huduma bora, rahisi na zinazozingatia mahitaji ya wateja.
Wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki matembezi ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja 2026 jijini Dar es Salaam, yenye kaulimbiu “The Extra Mile”, wakionesha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kutoa huduma bora, yenye ufanisi na inayoweka wateja mbele.
……………..
Benki ya Exim Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 kwa kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora, zenye mwitikio na zinazomweka mteja mbele, kupitia kaulimbiu ya mwaka huu, “The Extra Mile.”
Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo, wafanyakazi wa Benki ya Exim walishiriki katika matembezi ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, yakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Jaffari Matundu, ikiwa ni ishara ya dhamira ya benki hiyo ya kumweka mteja katika kiini cha kila jambo linalofanywa.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Matundu alisema kwenda “The Extra Mile” kunamaanisha kumweka mteja kwanza na kuhakikisha kuwa kila mwingiliano na mteja unaongeza thamani kwake.
Alisisitiza kuwa huduma bora kwa wateja ni jukumu la pamoja ndani ya benki, ambapo kila mfanyakazi ana nafasi ya kuhakikisha huduma za kibenki zinakuwa rahisi, bora zaidi na zenye mwitikio kwa mahitaji ya wateja.
